Posts

Showing posts from August, 2017

Ali Kiba, Nandy, Bebe Cool na Nyashinski kuwania tuzo za AFRIMA

Wanamuziki wa Tanzania, Uganda na Kenya akiwemo Ali Kiba, Nandy, Bebe Cool na Nyanshiski ni miongoni mwa nyota 18 wa muziki walioteuliwa kuwania tuzo za All Africa Music Awards {AFRIMA} zinazotarajiwa kuandaliwa mnamo mwezi Novemba. Wengine walioteuliwa ni pamoja Bebe Cool wa Uganda , Yemi Alade, AKA, Runtown, Nasty C, Eddy Kenzo, Locko, Anselmo Ralph, Jah Prayzah, Busiswa, Amanda Black, Kiff No Beat, Mafikizolo, Micasa na Olamide. Orodha ya walioteuliwa ilitangazwa mwezi Agosti katika hoteli ya Renaissance mjini Lagos, Nigeria. Orodha ya walioteuliwa ina makundi 33, ikiwemo 10 ya kieneo mbali na mengine 23 huku nyota wa Coke studio wakijizolea nafasi 25. Katika tuzo nyengine ya Afrima ya baadaye nyota wengine wa Coke studio wameteuliwa katika kundi la kibara. Wao ni Kiff No Beat (Ivory Coast) Mafikizolo na Mi Casa kutoka Afrika Kusini katika kundi bora la muziki Afrika. Kwa kundi bora zaidi barani Afrika walioteuliwa ni Anselmo Ralph (Angola) na Alikiba (Tanzania). ...

Mambo aliyoyafanya Donald Trump wakati wa likizo

Kwenye mambo yako, huwezi kukosa kuyajumuisha haya ambayo wewe kama Trump na wenzako White House mmekuwa wakifanya, ambayo ni yafuatayo: Alimwajiri mkurugenzi mpya wa mawasiliano kwa jina Anthony Scaramucci Mkuu wake wa mawasiliano na wanahabari Sean Spicer ajiuzulu. Alisema anafurahia hatua hiyo lakini alionekana mwenye hasira The Mooch (aka Scaramucci) alifanya mahojiano yasiyo ya kuridhisha na jarida la New Yorker Trump amfuta mkuu wake wa utumishi wa umma Reince Priebus (ambaye aliachwa kambi ya jeshi la wanahewa ya Andrews) Amwajiri mkuu mpya wa utumishi wa umma, Jenerali Kelly, ambaye alikuwa mkuu wa usalama wa ndani Siku ya kwanza ya Kelly kazini, rais alimfuta kazi mkurugenzi wake mpya wa mawasiliano - Scaramucci aliyekuwa kazini siku 10 pekee. Amwajiri mkurugenzi mpya wa mawasiliano, wa nne katika miezi saba. Anamwaibisha hadharani mwanahesria wake mkuu, mara kadha, lakini Jeff Sessions anaendelea kuvumilia Mswada wake wa huduma ya afya unashindwa bungeni Anawashu...

Upinzani waruhusiwa kukagua mitambo ya tume ya uchaguzi Kenya

Mahakama ya Juu nchini Kenya imeuruhusu muungano wa upinzani nchini humo National Super Alliance (Nasa) kupekua sava zilizotumiwa na tume ya uchaguzi nchini humo wakati wa uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti. Mahakama hiyo imesema muungano huo utaweza kusoma data kwenye sava hizo chini ya uangalizi kuhakikisha usalama wa mitambo ya IEBC hauhujumiwi. Mgombea wa Nasa Raila Odinga amewasilisha kesi mahakamani kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee. Mawakili wa Bw Odinga wameruhusiwa na mahakama kunakili data kutoka kwenye sava hizo kwa ajili ya kufanya uchunguzi kuhusu uchaguzi huo.

Mvutano kuhusu kufunguliwa kwa mitambo ya tume Kenya

Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Kenya imeendelea leo kwa siku ya pili katika mahakama ya juu zaidi ya taifa hilo, huku mahakama hiyo ikisikiliza hoja za upande wa washtakiwa. Mapema Mahakama hiyo ilipokea malalamiko ya mawakili upande wa upinzani NASA kwamba Tume ya uchaguzi (IEBC) ilikataa kuwapatia wataalam wake wa teknolojia ya mawasiliano fursa ya kuchunguza mitambo ya data ya tume hiyo ilizotumiwa kuhesabu kura za urais, kama ilivyoagizwa na mahakama Jumatatu. Upinzani umedai mitambo ya IEBC iliingiliwa ili kumpatia ushindi rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti, tuhuma ambazo tume hiyo imekanusha.