Mambo aliyoyafanya Donald Trump wakati wa likizo


Kwenye mambo yako, huwezi kukosa kuyajumuisha haya ambayo wewe kama Trump na wenzako White House mmekuwa wakifanya, ambayo ni yafuatayo:
  1. Alimwajiri mkurugenzi mpya wa mawasiliano kwa jina Anthony Scaramucci
  2. Mkuu wake wa mawasiliano na wanahabari Sean Spicer ajiuzulu. Alisema anafurahia hatua hiyo lakini alionekana mwenye hasira
  3. The Mooch (aka Scaramucci) alifanya mahojiano yasiyo ya kuridhisha na jarida la New Yorker
  4. Trump amfuta mkuu wake wa utumishi wa umma Reince Priebus (ambaye aliachwa kambi ya jeshi la wanahewa ya Andrews)
  5. Amwajiri mkuu mpya wa utumishi wa umma, Jenerali Kelly, ambaye alikuwa mkuu wa usalama wa ndani
  6. Siku ya kwanza ya Kelly kazini, rais alimfuta kazi mkurugenzi wake mpya wa mawasiliano - Scaramucci aliyekuwa kazini siku 10 pekee.
  7. Amwajiri mkurugenzi mpya wa mawasiliano, wa nne katika miezi saba.
  8. Anamwaibisha hadharani mwanahesria wake mkuu, mara kadha, lakini Jeff Sessions anaendelea kuvumilia
  9. Mswada wake wa huduma ya afya unashindwa bungeni
  10. Anawashutumu hadharani wanachama watatu wa Republican waliopinga mswada huo, mara kadha
  11. Apiga marufuku watu waliokumbatia jinsia tofauti kuhudumu jeshini, kupitia Twitter, bila kufahamisha jeshi
  12. Wakuu wa jeshi wamwambia: "Sahau, huwa hatupokei amri kupitia Twitter; kuna njia ya mawasiliano"
  13. Atoa hotuba ya kisiasa kwa maskauti wa miaka 11-18
  14. Adai kiongozi wa maskauti alimpigia simu kumpongeza kwa hotuba njema zaidi aliyowahi kuitoa
  15. Kiongozi wa maskauti asema hakumpigia simu kama hiyo, na kutoa taarifa kuwaomba radhi maskauti kwa sababu ya tamko hilo la rais
  16. Asema rais wa Mexico alimpigia simu kumpongeza kwa sera zake kuhusu mpaka
  17. Rais wa Mexico asema hakupiga simu kama hiyo
  18. White House yakanusha kwamba rais ni mwongo, lakini yashindwa kufafanua kuhusu madai ya rais
  19. Achukua siku nyingi kutia saini mswada wa vikwazo dhidi ya mataifa mengine (ikiwemo Urusi) na kisha alaumu bunge la Congress kwa kufanya autie saini
  20. Amshukuru Vladimir Putin kwa kuwatimua mamia ya wanadiplomasia wa Marekani
  21. Ashutumu wanaovujisha siri za Marekani lakini asema anapenda kuvujishwa huko kwa sababu humfanya watu wampende
  22. Awahimiza polisi wawe wakati wakati wanapokuwa wakiwakamata washukiwa
  23. Wakuu wa polisi washutumu taarifa hiyo. White House wafafanua kwamba ulikuwa mzaha
  24. Amuaibisha hadharani kiongozi wa chama cha Republican katika bunge la Senati, ambaye anamhitaji sana ili mambo mengi yake yapitishwe, mara kadha.
  25. Aonekana kuijibu Korea Kaskazini kwa kutishia vita vya nyuklia
  26. Awaambia wakazi wa kisiwa cha Guam, ambacho kina kambi kubwa ya kijeshi ya Marekani, ambacho Korea Kaskazini ilikuwa imetishia kushambulia, kwamba hilo litasaidia utalii
  27. Mkuu wake wa mikakati Steve Bannon atoa tamko la kukinzana. Asema: "Hakuna mpango wowote wa kuingilia kijeshi Korea Kaskazini"
  28. Atishia Venezuela kwamba anaweza kutumia jeshi kuingilia kati
  29. Baada ya mkutano wa watetezi wa ubabe wa wazungu, ambapo mwanamke mmoja aliuawa, rais alaumu pande zote mbili
  30. Baada ya kushutumiwa sana, ajirekebisha. Awashutumu watetezi wa ubabe wa wazungu, wafuasi wa siasa za Nazi na wanachama wa kundi la Ku Klux Klan
  31. Huku akiwa na hasira kwa sababu ya kulazimishwa kujirekebisha, abadilisha mambo na kurejelea kulaumu pande zote mbili na kusema kwamba kuna watu wazuri katika makundi yote.
  32. Wakuu wa jeshi watoa taarifa ambapo walishutumu aina zote za ubaguzi, katika hatua iliyoonekana kama kumshutumu amiri jeshi mkuu
  33. Apigia debe shaba lake la mizabibu Virginia alipoulizwa iwapo yeye - kama rais - atazuru Charlottesville
  34. Hatua iliyomfanya kushutumiwa na viongozi wa Democrat, Republican, marais wa zamani, viongozi wa nchi nyingine duniani, washirika wake, wafanyakazi wake na hata Papa Francis mwenyewe.
  35. Awadhalilisha hadharani wakuu wa kampuni waliokuwa wakijitenga naye. Wakuu watendaji wengine wa kampuni waondoka kwenye baraza lake la washauri muhimu White House
  36. Amfuta kazi Steve Bannon, mkuu wake wa mikakati ambaye alikuwa mkuu wake wa kampeni na aliyesaidia sana ushindi wake
  37. Apiga 'U-turn' kuhusu Afghanistan na kuahidi kutuma wanajeshi zaidi, bila kujali kwamba alikuwa awali amesema mara nyingi kwamba angeondoa majeshi ya Marekani nchini humo
  38. Atishia kuifunga serikali iwapo hatapata ufadhili wa ujenzi wa ukuta mpaka wa Marekani na Mexico
  39. Awaomba watu wa Marekani kuonyesha umoja
  40. Siku iliyofuata, washutumu vikali maadi na wakosoaji wake katika hotuba iliyowagawanya wengi
  41. Siku moja baadaye, ahimiza umoja
  42. Amsamehe liwali wa zamani wa Arizona Joe Arpaio, aliyekuwa amepatikana na kosa la kukaidi agizo la mahakama kwamba asitishe doria barabarani dhidi ya wahamiaji haramu.
Mkuu wa utumishi wa umma wa zamani wa Barack Obama ambaye sasa ni meya wa Chicago, Rahm Emanuel, wakati mmoja aliandika kwenye Twitter kwamba atapendekeza White House itunukiwe tuzo ya sanaa ya Tony kwa kuwa na hadithi ya kuchekesha zaidi.

Comments

Popular posts from this blog

Tabia za Watu na Alama za Nyota

BANK LAW NOTES

ADMINISTRATIVE LAW