Posts

Showing posts from April, 2017

Marekani yatumia bomu kubwa zaidi kushambulia IS

Image
Jeshi la Marekani kwa mara ya kwanza limewashambulia wapiganaji wa kundi la Islamic State kwa kutumia bomu kubwa lisilokuwa la nyuklia, kuwahi kutumiwa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani, katika vita. Bomu hilo aina ya GBU-43 ambalo limetumika kutekeleza shambulio hilo, kipimo chake cha nguvu kilichotumika kinalingana sawa na tani 11 za TNT, na ambalo pia hujulikana kama ''Mama wa mabomu yote'' lilipigwa katika mapango yanayotumiwa na wapiganaji wa Islamic State kujificha katika jimbo la Nangarhar, mashariki mwa Afghanistan. Akielezea kulipuliwa kwa bomu hilo ardhini Gavana katika Wilaya ya Achin jimboni humo, Esmail Shinwari amesema ni kama vile miale mikali ilimeza eneo hilo. Mkuu wa kikosi cha jeshi la Marekani nchini Afghanistan, Jenerali John Nicholson amesema bomu hilo lilikuwa ni zana sahihi kutumika kuendeleza kasi ya kupambana na waislamu hao wenye itikadi kali. Akitoa taarifa Msemaji wa Ikulu ya Marekani Sean Spicer amesema tahadhari zilichukuliwa kupungu...

Rais Magufuli alaani mauaji ya polisi 8 Tanzania

Image
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na kushutumu mauaji ya polisi wanane wa taifa hilo waliouawa na watu wasiojulikana jioni siku ya Alhamisi. Katika taarifa kwa vyombo vya habari wanane hao walikuwa wakitoka kubadilishana doria waliposhambuliwa kwa kupigwa risasi katika eneo la Jaribu mpakani mwa wilaya ya Kibiti mkoani Pwani. Walikuwa wakisafiri kwa gari katika barabara ya Dar es Salaam na Lindi.  Magufuli amelaani tendo hilo na matukio yote ya kuwashambulia polisi akisema wanafanya kazi kubwa ya kuwalinda raia. Ametuma rambirambi kwa jamaa na marafiki walioguswa na vifo hivyo huku akiwataka raia wote kushirikiana katika kukomesha vitendo kama hivyo. ''Nimeshtushwa na nimesikitishwa sana na vifo vya asakari wetu 8 ambao wamepoteza maisha wakiwa wanalitumikia taifa, naungana na familia za marehemu wote, jeshi la polisi na Watanzania wote katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na majonzi ya kuondokewa na vijana wetu shupavu,namuomba mungu atupe myo ...

Dkt. Rais Magufuli katika uzinduzi wa hostel UDSM

Image
watch it here

Waarabu wamsifu 'Abu Ivanka' almaarufu rais Donald Trump kwa mashambulizi dhidi ya Syria

Image
Waarabu katika mitandao ya kijamii wamem'miminia sifa tele rais wa marekani Donald Trump na shukrani na shangwe baada ya kuamrisha shambulizi la kwanza la kijeshi kutoka Marekani dhidi ya vikosi vya serikali ya Syria. Marekani ilifanya mashambulizi hayo dhidi ya kambi ya jeshi la wanahewa katika majira ya asubuhi siku ya Ijumaa kufuatia shambulizi linalokisiwa kuwa la kemikali katika jiji linaloshikiliwa na waasi. Muda mfupi baadaye, baadhi ya Waarabu wanaotumia mitandao ya kijamii walianza kumtaja Rais Trump kama 'Abu Ivanka' - au babake Ivanka, kama onyesho la heshima kwake Wengine walimuita Abu Ivanka al-Amreeki - au babake Ivanka Muamerika, akiwa amefuga ndevu. Lakini kuna wale walioshuku mwelekeo wa rais huyo na nia yake. Mtumizi mmoja alimpa Trump sura mpya akitumia picha yake akiwa amevalia kofia ya utamaduni iitwayo tarboosh, na maandishi: " Tunakupenda" Pia alitajwa kama mtu anayesema na kutenda, huku mtumizi mmoja akimuambia alifanya kwa mud...

Tabia za Watu na Alama za Nyota

Image
Tabia za Watu na Alama za Nyota Alama za nyota zinabashiri tabia na haiba ya binadamu katika dunia. Mpangilio au nafasi ya sayari katika mzunguko wake angani unaaminika kuleta athari kwa binadamu na matukio katika dunia. Kuna alama 12 za kiastrolojia. Kila moja ina mvuto wa nguvu wa kipekee toka katika nyota. Alama hizi ni kama ifuatavyo: Samaki  (Pisces):Feb 19 – Machi 20 Kondoo  (Aries): Machi 21 – Aprili 19 Ng’ombe  (Taurus): Aprili 20 – Mei 21 Mapacha :(Gemini ): Mei 22 – Juni 20 Kaa (Cancer): Juni 21 – Julai 22 Simba (Leo): Julai 23 – Agosti 22 Mashuke (Virgo):Agosti 23 – Sept 22 Mizani  (Libra): Sept 23 – Okt 22 Ng’e  (Scorpio): Okt 24- Nov 21 Mshale  (Sagittarius): Nov 22- Des 21 Mbuzi (Capricorn):Des 22 – Jan 19 Ndoo  (Aquarius):Jan 20 – Feb 18 Makundi ya Alama za Nyota: Alama hizi 12 za nyota zinagawanyika katika elementi 4 zijulikanazo kama: Moto: Yenye matamanio ya mafanikio au makuu,dadisi Maji: Yenye kubadilika ...

Alichoandika Wema Sepetu kwa ukurasa wake wa Instagram kuhusu Roma

Image
wemasepetu This Is Scary... Ni Janga kubwa sana kwa wasanii, kwa wananchi na Kwa Taifa letu kiujumla... Kinachonishangaza ni kuona baadhi ya wasanii wa Bongo movie wamekazana kupost eti wapo kwa Mkuu wa mkoa wakiongelea WaKorea na Waphilipino.... Mlikumbuka kumuuliza Mheshimiwa alipo Roma na Moni...??? Au ndo mambo ya kila mtu anaangalia lake.... Au labda mpaka atekwe msanii wa Bongo movie pia ndo akili itatukaa sawa...??? Oh God help Us Please... Lakini pia wala sitoshangaa hata kama akitekwa msanii wa bongo movie hakuna atakaehangaika within Us zaidi ya wananchi peke yao na watu wetu wa karibu... Tumejawa sana Unafki...!!! All in All namuonea sana huruma Nancy.... Our prayers are with u mama... Inshallah mumeo atapatikana... Tuzidi kumuomba Mungu.....🙏🏼🙏🏼🙏🏼.... Kabla sijasahau, Tuwage tuna hata fikra za kujua tupo kwenye wakati gani na tupost vitu gani....!!! Yaani mtu kapotea siku ya pili mko busy na kupost Wakorea na Waphilipino...?? 🙄🙄🙄 SMH..

Mkuu wa Mkoa Paul Mkonda amesema waliomteka Roma wajiandae

Image
watch it here

Gumzo mitandaoni kuhusu Msanii Roma Mkatoliki kutoweka Tanzania

Image
Msanii wa bongo Fleva kutoka Tanzania Ibrahim Musa aka Roma Mkatoliki ametoweka baada ya kudaiwa kukamatwa mapema siku ya Alhamisi katika mji wa Dar es Salaam. Inadaiwa alichukuliwa katika studio moja katika mji huo pamoja na mtayarishaji wake. Ripoti nyengine zinasema kuwa vifaa vyake vya kurekodi pia vilichukuliwa. Raia wamekuwa wakisambaza habari katika mtandao wa Twitter: Familia za wawili hao zinasema kuwa zimetembelea vituo vya polisi ,lakini hazijaweza kuwapata. Joff Msumule, rafikiye mzalishaji huyo amesema kuwa maafisa wa polisi walikuwa wanatafuta ushahidi wa kuwashtaki wanamuziki hao. Sikuwepo lakini naeleza kwamba kulikuwa na wimbo uliotayarishwa ambao inadaiwa hautoi ujumbe mzuri kwa serikali. Wimbo huo haukurekodiwa katika studio ya Tongo, lakini msanii alitumia chapa ya studio hio. Hii inamaanisha kwamba sisi ndio tuliourekodi wimbo huo kwa hivyo maafisa wa polisi walikuja kuchukua ushahidi. Joseph Mbilinyi msanii wa zamani ,ambaye kwa sasa ni mbunge al...

vituko vya kitale

Image