Trump kulaani shambulio la kemikali yenye sumu,Syria

Marekani na mataifa mengine ya magharibi yamemshutumu Rais wa Syria, Bashar Assad na serikali yake kwa kile walichodai shambulio la kutumia silaha za kemikali la siku ya jumanne mjini Khan Sheikhoun.
Trump amesema vifo vya watoto vimebadili mtazamo wake kwa Assad.

''na nitakueleza, kuwa shambulio lile dhidi ya watoto limenifanya niwe na mtazamo mwingine. Ni kitu cha kutisha inatisha sana, na nimekuwa nikifuatilia na kutazama, hakuna namna nyingine zaidi naweza kusema, imekwishatokea kuwa sasa mtazamo wangu kwa Syria na Assad umebadilika sana.''

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tillerson ambaye anatarajiwa kufanya ziara mjini Moscow nchini Urusi juma lijalo, ameitaka Urusi ifikiri kwa makini kuhusu uhusiano wake na Syria
hakuna shaka yeyote kuwa utawala wa Syria chini ya Bashar Al Assad unahusika na shambulio hili la kinyama na tunaona sasa ni wasaa kwa warusi kufikiri kwa makinni kwelikweli kuhusu kuendelea kuunga mkono utawala wa Assad''
Urusi imepinga msimamo wa marekani na mataifa ya magharibi kuhusu tukio hilo na kusema kuwa , mswada kuhusu azimio la baraza la usalama la umoja wa mataifa kuhusu shambulio hilo ni chuki dhidi ya Syria.
Comments
Post a Comment