Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, amemwagiza kamanda wa polisi Mkoa wa Mtwara, Lucas Mkondya kumuweka ndani ofisa kazi wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote, Nadhiru Omary kwa madai ya kushindwa kutatua malalamiko ya wafanyakazi ambayo yanaelekezwa katika ofisi yake. Byakanwa ametoa maagizo hayo leo Jumatano, Jana Machi 7, alipofika kiwandani hapo baada ya baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho kugoma kuendelea na kazi kwa muda usiojulikana kwa madai mbalimbali. Wafanyakazi hao wanadai kunyanyaswa, kutolipwa mishahara yao kwa wakati na kufukuzwa kazi bila kuzingatia sheria. “Tangu nimefika hapa wewe bwana umelaumiwa na umetuhumiwa kwa mambo mengi,hata vikao vyote tulivyokaa hujabadilika, kwa sababu kama ungebadilika taarifa hizi tungezijua mapema,” alisema na kuongeza kuwa: “Sisi kama Serikali tungekaa na watumishi hawa kabla hawajaanza kuandamana, RPC huyu akapumzike kwanza, kamata huyu mtu tuondoke naye hatuwezi kuendelea na watu ambao badala ya kusikiliza mal...