Tetesi za soka Ulaya
Mshambuliaji wa klabu ya Psg ya
Ufaransa Mbrazil Neymar anajutia kuondoka katika klabu ya Barcelona na
taarifa zinasema anataka kurejea klabuni hapo mwaka 2019 . (Mundo
Deportivo - in Spanish)
Manchester City wako tayari kuingia katika
mbio za kumsajili kiungo Thomas Lemar mwenye umri wa miaka 22 kutoka
klabu ya Monaco ya Ufaransa.(Telegraph)
Klabu ya Manchester United
iko katika mawindo ya kutaka kumsajili mlinzi wa Fc Barcelona Samuel
Umtiti's ambaye dau lake la kuuzwa ni pauni milioni 54.(Talksport)
Pia
United wanataka kumsajili beki Sokratis Papastathopoulos, anayekipiga
katika klabu ya Borrusia Dortmund na wamekuwa wakimfuatilia kwa ukaribu
wiki hizi za karibuni . (Mirror)
Kiungo wa Chelsea Na Timu ya
taifa ya Ufaransa Ngolo Kante amesema anavutiwa kidogo sana na kutaka
kujiunga na miaka ya soka la Ufaransa .
Klabu ya Paris St-Germain
licha ya timu hiyo kumfanya Ngolo Kante kuwa ndio mchezaji anayatakiwa
kusajilia zaidi katika dirisha kubwa la usajili (London Evening
Standard)
Beki kisiki wa Arsenal Hector Bellerin, 22, anakaribia kujiunga na Juventus ya nchini Italia. (Bleacher Report, via Mirror)
Mshambuliaji
wa Bayern Munich,Robert Lewandowski yuko huru kuweza kujiunga na Real
Madrid hata hivyo Chelsea pia wako mstari wa mbele kuhakikisha wanaoata
saini ya mchezaji huyo raia wa Poland. (Bleacher Report)
Meneja wa
timu ya taifa ya England Gareth Southgate yuko tayari kumpata
mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane kitambaa cha unahodha wa timu ya
taifa katika michuano ijayo ya Kombe la dunia(Star)
West Ham
inamuwinda kiungo wa Klabu ya Trabzonspor,Okay Yokuslu. Mwenye umri wa
Miaka 23 kiungo huyu pia anawaniwa na Sevilla ya Hispania (AS - in
Spanish)
Timu ya West Brom pia wanamfutilia mchezaji Okay
Yokuslu, ambae ameichezea timu ya taifa ya Uturuki Mara tano (Milliyet -
in Turkish)
Paris St-Germain Inataka kumarisha Safu yake ya
ulinzi haswa upande wa kushoto kwa kutaka kuwasajili kinda wa Kingereza
Ryan Sessegnon, mwenye miaka 17, Pamoja na Mbrazil Alex Sandro kutoka
Juventus(Talksport)
Brighton wameungana na Crystal Palace na
West Ham katika mbio za kumuwania kiungo wa Lille ya Ufaransa Ibrahim
Amadou, 24. (Le10 Sport, via Sun)
Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere, 26 amesema hajakaribia kusaini
mkataba mpya huku mkataba wake wa sasa unafikia mwisho ndani ya muda wa
miezi mitatu ijayo. (Independent)
Mshambuliaji wa Everton Sandro
Ramires ambae anachezea klabu ya Sevilla kwa Mkopo amesema anataka
kusalia Sevilla kwa mkataba wa kudumu, Sandro alipelekwa klabuni hapo
kwa mkopo mwezi januari. (Liverpool Echo)
Comments
Post a Comment