Mbunge Elibariki Kingu: Watu kutekwa na kuuawa ni kawaida, haina haja ya kulipeleka Bungeni
Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu amesema suala la bunge kujadili hali ya usalama wa nchi na kutaka kamati iundwe kuchuguza matukio mbalimbali ya kihalifu kutasababisha hali ya taharuki ambayo tafsiri yake ni kama serikali imeshindwa kusimamia usalama wa nchi.
Mbunge huyu anapinga hatua ya hatua ya Bashe kusema atapeleka hoja binafsi bungeni kuhusu kuundwa kamati ya kujadili jambo hili.
"Matukio ya utekajitekaji, mtu aliyetekwa ikavuma sana ilikuwa msanii Roma, Vyombo vya Polisi vina wajibu wa kutuambia leo ni nani kamteka Roma.Lakini isipelekee tujenge twasira kwamba hii nchi sasa imeshakuwa sasa Dah...Ndugu zangu mimi nmeishi Uganda, Usalama wa nchi ya kwetu ni wa hali ya juu jamani.Nmeishi Kenya, Nmeishi Rwanda, Nmeishi nchi mbalimbali nmeishi Afrika kusini nmeishi Botswana nmeishi china, nmeishi nchi mbalimbali, Usalama wa kwetu jamani bado ni mkubwa. Hakuna ubaya, Bunge linaweza kujadili jambo lolote kwa sababu ndo kazi yake ya kikatiba.bunge hilo mimi sina mamlaka ya kulizuia rais hana mamlaka ya kulizuia sababu ni Mamlaka ya watu. Lakini bado ninaona Usalama wa nchi yetu so far, changamoto ndogondogo hizi hakuna taifa linalokosa changamoto.
Kipindi cha Jakaya kuna matukio yalitokea makubwa sana watu waling'olewa meno.Kuna Dr. Olimboka aling'olewa meno,Wakina Kibanda mwandishi mkubwa nguli aling'olewa macho mpaka sasa hivi Kibanda hana macho. Hakunataifa linaweza likaenda bila ya kuwa na uhalifu.Na hii ni changamoto kwa Serikali. Lakini mimi kama Mbunge, Mimi ni Mbunge wa CHama cha Mapinduzi na najua Serikali yangu haijashindwa.Lakini jeshi la Polisi liwe na Uharaka wa kutoa taarifa na ripoti.Lakini tukienda Bungeni tunaenda kuleta taharuki kwamba sasa Serikali imeshindwa kudhibiti hali.Kitu ambacho Bunge linakijadili, ilijadili bunge linakuja na azimio, Mimi sidhani kama tumefika hiyo hatua.Matukio haya kila utawala yanakuwepo.Polisi hawana Maadili, Rais hawezi kumtuma Polisi akampige risasi Mwananfunzi, lakini tunailaumu serikali. Siamini kama Serikali yangu imeshindwa hadi tuanze kuiwajibisha bungeni". Amesema Kingu
Comments
Post a Comment