Trump afanya maamuzi mwenyewe kukutana na kiongozi wa Korea kaskazini

Rais Trump ameandika kwenye ukurasa
wake wa mtandao wa kijamii wa Twittter kuwa makubaliano na Korea
Kaskazini yapo kwenye mchakato wa kutekelezeka ,
siku moja baada ya kukubali kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
Ingawa mpaka sasa Korea Kaskazini haijatoa tamko lolote.
Aidha
Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence amesema uamuzi wa Korea
Kaskazini kutaka kukutana na rais wa Marekani Donald Trump unathibitisha
kuwa mpango wa kuitenga Korea Kaskazini unafanya kazi.
Hata hivyo makuliano ya mkutano huo wa kihistoria uliwashangaza waangalizi.
Lakini
badae ikulu ya white house ya Marekani imesema mkutano huo hauwezi
kufanyika mpaka Korea Kaskazini ichukue hatua thabiti kabla ya mkutano
wowote.
Mwezi mmoja tu uliopita ,rais Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un walikuwa wana malumbano makali.
Lakini sasa rais Trump amekubali kuhudhuria mkutano huo alioalikwa licha ya kuwa mwaliko huo uliletwa na Korea kusini.
Vyombo vya habari vya Marekani vinataarifu kuwa rais Trump alifanya
maamuzi ya kuhudhuria mkutano huo bila kupata ushauri wowote katika
utawala wake.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson
ambaye yuko kwenye ziara yake ya kwanza barani Afrika amethibitisha kuwa
maamuzi hayo yalikuwa ya Trump peke yake na yeye hakufahamu lolote juu
ya hilo licha ya kuwa walikuwa na mazungumzo kabla ya tangazo hilo
kutolewa.
Ingawa ujumbe huo wa kukaribishwa kwa Trump umekuwa
unajichanganya kwa kuwa katibu wake Trump Sarah Sander aliwaambia
waandishi wa habari kuwa Korea Kaskazini imehaidi kusitisha mpango wake
wa nuklia na wamekubali kufanya hivyo kabla ya mkutano huo.
Trump
atakuwa kiongozi wa kwanza wa Marekani kukutana na kiongozi wa Korea
Kaskazini kama mkutano huo utaafikiwa kwa kuwa hakuna kiongozi wa
Marekani aliyewahi kukutana na kiongozi wa Korea kaskazini . READ MORE ON http://www.bbc.com/swahili/habari-43355504
Comments
Post a Comment