Tanzania na Burundi miongoni mwa nchi ambazo raia hawana furaha duniani kwa mujibu wa UN 2018
Tanzania, Burundi na Rwanda
zimeorodheshwa kuwa kati ya nchi zenye watu wasio na furaha duniani
katika orodha ya kila mwaka ya Umoja wa Mataifa kuhusu viwango vya
furaha duniani.
Burundi ndilo taifa ambalo wakazi wake hawana
furaha zaidi duniani katika nafasi ya 156 ambapo imechukua nafasi hiyo
kutoka kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) iliyokuwa inashikilia nafasi
hiyo mwaka jana.
CAR ndiyo inayoifuata Burundi katika orodha ya mwaka huu.
Tanzania
imeshika nafasi ya 153 sawa na mwaka jana huku Rwanda pia ikishikilia
nafasi ya 151 sawa na mwaka jana kati ya mataifa 156.
Orodha ya mwaka jana hata hivyo ilishirikisha mataifa 155.
Taifa
linaloongoza kwa furaha duniani mwaka huu ni Finland, kwa mujibu wa
ripoti hiyo ya UN ambapo nchi hiyo imechukua nafasi hiyo kutoka kwa
Norway.
Ripoti hiyo huangazia furaha waliyo nayo watu wa taifa furahi na chanzo cha furaha hiyo.
Mataifa ya Ulaya Kaskazini yanashikilia nafasi tano za juu kwa kuwa na
viwango vya juu vya raia walioridhika, huku nchi zilizoathiriwa na vita
vya muda mrefu pamoja na nchi kadha za Afrika Kusini mwa Sahara
zikiendelea kwa mara nyingine kushikilia nafasi tano za chini.
Burundi, taifa ambalo raia hawana furaha zaidi, lilitumbukia kwenye
mzozo wa kisiasa baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuamua kuwania tena
urais kwa muhula wa tatu mwaka 2015. Mwaka huo kulitokea pia jaribio la
mapinduzi ya serikali.
Nchi zenye watu walio na furaha na wasio na furaha Duniani mwaka 2018 | |
---|---|
Nchi zenye watu walio na furaha Duniani | Nchi zenye watu wasio na furaha Duniani |
1. Finland |
147. Malawi |
2. Norway |
148. Haiti |
3. Denmark |
149. Liberia |
4. Iceland |
150. Syria |
5. Switzerland |
151. Rwanda |
6. Netherlands |
152. Yemen |
7. Canada |
153. Tanzania |
8. New Zealand |
154. South Sudan |
9. Sweden |
155. Central African Republic |
10. Australia |
156. Burundi |
Orodha hiyo huaandaliwa kwa kuangazia pato la
mtu kwa kila mwaka, miaka ambayo mtu anatarajiwa kuishi, kuwa na mtu wa
kutegemea kwa usaidizi, dhana ya kuwepo uhuru wa kufanya maamuzi
maishani, uhuru kutoka kwa ufisadi, na ukarimu miongoni mwa mengine.
Imetayarishwa na shirika la maendeleo endelevu, Sustainable Development Solutions Network (SDSN), ambalo lilianzishwa na Umoja wa Mataifa.
Mwaka 2017, hali ilikuwa hivi:
Nchi zenye watu walio na furaha na wasio na furaha Duniani mwaka 2017 | |
---|---|
Nchi zenye watu walio na furaha Duniani | Nchi zenye watu wasio na furaha Duniani |
1. Norway | 146. Yemen |
2. Denmark | 147. Sudan Kusini |
3. Iceland | 148. Liberia |
4. Uswizi | 149. Guinea |
5. Finland | 150. Togo |
6. Uholanzi | 151. Rwanda |
7. Canada | 152. Syria |
8. New Zealand | 153. Tanzania |
9. Australia | 154. Burundi |
10. Sweden | 155. Jamhuri ya Afrika ya Kati |
Comments
Post a Comment