ABDUL NONDO APATIKANA IRINGA NA JESHI YA POLISI LA AHADI KUMSHUGHULIKIA
https://www.youtube.com/watch?v=5AkauY6tEA0
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi
nchini Tanzania , Abdul Nondo ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar
es Salaam aliye ripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha
amepatikana akiwa hai eneo la Mafinga mkoani Iringa kusini magharibi
mwa nchi hiyo.
Inadaiwa kuwa alijikuta katika eneo hilo baada ya
kuzinduka kutoka katika lindi la usingizi na kuwauliza wenyeji wa eneo
alilo jikuta kuwa yuko wapi? ambao walimfahamisha kuwa yuko Mafinga
mkoani Iringa na kisha akapelekwa kituo cha polisi kilichoko karibu.Mahojiano yake katika kituo cha Polisi Mafinga eneo alikopatikana yamefanyika na baadaye kupiga simu kwa ndugu zake. Baada ya kupata taarifa ya kupatikana mwanawe, baba mzazi Mussa Mitumba ameomba namba za askari aliyemfanyia mahojiano ili kujua nini kilimpata mwanae ili aweze kujua kama jambo jingine alilowaambia kuhusiana na kutekwa kwake.
Alionekana mara ya mwisho mnamo Jumanne katika afisi za shirika hilo eneo la Sinza, Dar es Salaam alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyokuwa imetolewa na shirikisho la vyuo vikuu nchini humo, Tahliso.
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) ulisema baada ya kuondoka afisi hizo, Bw Nondo alielekea chuoni na kuaga kuwa anaondoka kwenda nyumbani Madale.
Awali kabla ya tukio hilo mwanafunzi huyo alielezea kwamba alikuwa akifuatiliwa mara kadhaa watu asiowatambua na wenye nguo za kiraia wakijitambulisha kama watu wa usalama ambao wamekuwa wakimpatia vitisho.
Comments
Post a Comment