Dele Alli: Kiungo wa Tottenham afungiwa kwa mechi tatu Ulaya
Mchezaji wa kiungo wa kati wa Tottenham Dele Alli amefungiwa kwa mechi tatu na shirikisho la soka Ulaya baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu wakati wa mechi dhidi ya timu ya Gent uwanjani Wembley mwezi wa Februari.
Alli alipewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Brecht Dejaegere, timu zote zilipotoka sare ya 2-2.
Iwapo Spurs watafanikiwa kunyakua tiketi ya moja kwa moja ya michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao, Alli atakosa nusu ya michuano yao ya makundi.
Spurs, iliyoondolewa katika ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League, na Gent.
Kwa sasa ni ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya England ikiwa imebakiza mechi 10.
Alli alikosa kucheza mechi tatu zilizopita za ligi kuu Uingereza baada ya kupatikana na hatia ya kumchezea visivyo mwenzake wa West Bromwich Albion Claudio Yacob.
Wakati huo huo , Arsenal imetozwa faini ya pauni elfu 4,300 baada ya baadhi ya mashabiki wake kuvamia uwanja wakati wa kichapo cha 5-1 wakiwa nyumbani dhidi ya Bayen Munich.
Shirikisho la soka Ulaya UEFA pia liliitoza faini ya pauni elfu 2,600 timu ya Bayern Munich kufuatia mashabiki wake kusababisha mechi kwenye uwanja wa Emirates kuchelewa kwa muda kwa kurusha karatasi za kutumiwa chooni, uwanjani kama njia ya kupinga bei ya juu ya kiingilio.
Timu nyingine iliyoadhibiwa ni Saint-Etienne kwa kupigwa faini ya pauni 43,000 baada ya mashabiki wake kurusha chupa na fataki uwanjani wakati wa mechi yao ya ligi ya Europa dhidi ya Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford mwezi uliopita.
Comments
Post a Comment