Waziri ashutumu askari kwa kuchomoa bastola wakimdhibiti Nape Nauye
Waziri wa mambo ya ndani nchini Tanzania Mwigulu Nchemba ameshutumu kitendo cha askari mmoja kuchomoa bastola na kufyatua risasi wakati maafisa wa usalama walipokuwa wanajaribu kumzuia aliyekuwa waziri wa habari kuhutubia wanahabari.
Bw Nchemba, kwenye ukurasa wake wa Facebook, amesema kitendo hicho si cha busara na kwamba afisa mhusika kuadhibiwa.
Amesema amemwagiza mkuu wa jeshi la polisi kutumia picha zilizopigwa wakati wa tukio hilo kumsaka mhusika."Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni Mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana rekodi ya uhalifu. Kitendo cha mtu kumtolea bastola, sio cha kiasikari, sio cha Kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa bastola mbele ya kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini," ameandika.
"Nahusika na usalama wa raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake.
Comments
Post a Comment