Wanaume wakutana White House 'kujadili wanawake' Marekani

Mike Pence na jopo la uhuru

Picha kama hii si geni na inafahamikana huenda ingeweza kuchukuliwa katika vyumba mbali mbali vya mikutano katika maeneo mbali mbali duniani - wanaume wakiwa wamezunguka meza wakipanga mipango na kujadili mkataba
Lakini ukosefu wa wanawake hapa, miongoni mwa kundi la wahafidhina wa Republican wakijadili mswada wa afya na makamu wa rais, ni suala la kushangaza.
Hii ni kwa sababu moja ya mambo yaliyojadiliwa ilikuwa ni ikiwa muswada huo unapaswa kuweka sharti kwamba mipango ya bima ya afya itoe "faida muhimu" zikiwemo huduma za uzazi.
Mwezi Januari, Ikulu ya White House ilikabiliwa na ukosoaji mkubwa pale Rais Trump alipo saini mswada wa utoaji mimba akiwa amezingirwa na wanaume.
Si ajabu kwamba wengi walianza kulalamika punde makamu wa rais Mike Pence alipotuma picha kupitia Twitter, yenye ujumbe: "Nashukuru kujiunga na @POTUS kwa mkutano na Freedom Caucus tena leo. picha hii. #PitishaMswada"
Seneta wa chama cha Democratic Pat Murray alikuwa mmoja wa watu wa kwanza kumjibu makamu wa rais akitoa tathmini kali juu ya picha hiyo
Patty Murray tweet: A rare look inside the GOP's women's health caucusHaki miliki ya pichaTWITTER
Lakini si wanawake pekee waliokerwa na picha hiyo.
Mbunge wa Congress Jim McGovern aliielezea kama ya kushangaza na kuudhi
Jim McGovern tweet: Haki miliki ya pichaTWITTER
Wengine walitoa maelezo ya kuonyesha namna picha hiyo haifai kulingana na hali halisi.
Haki miliki ya pichaTWITTER
Rais Trump amekuwa makini sana kuwajumuisha wanawake katika picha anazopigwa wakati akisaini sheria, tangu ikulu ya White House ilipokosolewa vikali kwa kupiga picha zote peke yake akisaini sheria ya utoaji mimba, katika siku yake ya kwanza mamlakani.
Chini ya wabunge watano wa Republican katika bunge la wawakilishi ni wanawake, lakini uwakilishi wa jinsia si tatizo tu la upande wa Republican - Bunge la Congress kwa ujumla bado lina wanaume wengi.
Wabunge wanawake ni 20% pekee.
Marekani inalinganishwa na Bangladesh inapokuja katika suala la uwakilishi wa wanawake bungeni.
Nchini Sweden uwakilishi wa wanawake ni wa 44%.
Wanaume wakizindua baraza la wasichana katika jimbo la Qassim nchini Saudi ArabiaHaki miliki ya pichaQASSIM GIRLS COUNCIL
Image captionKulikuwa na jumla ya wanaume 13 ( baadhi yao hawamo pichani ) ukumbini katika uzinduzi wa baraza la wasichana la Qassim nchini Saudi Arabia
Marekani sio taifa pekee kuwa na picha ya wanaume pekee wakichukua maamuzi yanayowahusu wanawake na kuibua mjadala.
Wiki iliyopita, uzinduzi wa baraza la wasichana katika jimbo la al-Qassim nchini Saudi Arabia ulilaaniwa wakati picha ya kwanza ilionyesha wanaume 13 wakiwa pamoja baada ya kuanzishwa kwa baraza la wasichana bila kuwemo hata mwanamke mmoja

Comments

Popular posts from this blog

Tabia za Watu na Alama za Nyota

BANK LAW NOTES

ADMINISTRATIVE LAW