MATAJIRI 25 AFRICA 2017
Mabilionea 25 matajiri zaidi Afrika 2017
Mfanyabiashara kutoka Nigeria Aliko Dangote bado ndiye mtu tajiri zaidi barani Afrika kwa mujibu wa orodha ya mabilionea mwaka 2017 iliyoandaliwa na jarida la Forbes.
Utajiri wa Dangote unakadiriwa kuwa jumla ya $12.2 bilioni.
Kuna mabilionea (wa Dola) 25 mwaka huu barani Afrika, mmoja juu ya 24 waliokuwepo mwaka jana.
Wafanyabiasha kutoka Nigeria Femi Otedola na Abdulsamad Rabiu hawakufanikiwa kuingia kwenye orodha hiyo mwaka huu.
Mtanzania Mohammed Dewji bado ndiye bilionea wa umri mdogo zaidi Afrika, utajiri wake ukikadiriwa kuwa $1.09 bilioni.
- Utajiri wa Trump washuka, Bill Gates aongoza
- Watu wanane matajiri kupindukia duniani
- Mtanzania afungua mgahawa Sweden
Isabel dos Santos kutoka Angola na mfanyabiashara wa mafuta Folorunsho Alakija kutoka Nigeria ndiye mabilionea wanawake pekee katika orodha hiyo mwaka huu.
Bw Dangote Dangote, ndiye mwanzilishi na mwenyekiti wa kampuni ya Dangote Cement inayoongoza kwa kuzalisha saruji Afrika. Anamiliki asilimia 90 ya hisa za kampuni hiyo.
Dangote Cement huzalisha tani 44 milioni za saruji kila mwaka na imepanga kuongeza uzalishaji kwa asilimia 33 kufikia 2020.
Dangote pia anamiliki hisa katika kampuni za chumvi, sukari na unga.
Mohammed Dewji ni afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya METL iliyoanzishwa na babake miaka ya 1970.
Kampuni hiyo huhusika katika biashara ya nguo, unga, vinywaji na mafuta.
Kampuni hiyo huendesha shughuli zake katika zaidi ya mataifa sita barani Afrika.
Mabilionea 25 wa Afrika mwaka 2017:
1. Aliko Dangote, Nigeria
Utajiri: $12.2 bilioni
2. Nicky Oppenheimer, Afrika Kusini
Utajiri: $7 bilioni
3. Mike Adenuga, Nigeria
Utajiri: $6.1 bilioni
4. Johann Rupert, Afrika Kusini
Utajiri: $6.3 bilioni
5. Nassef Sawiris, Misri
Utajiri: $6.2 bilioni
6. Christoffel Wiese, Afrika Kusini
Utajiri: $5.9 bilioni
7. Nathan Kirsch, Swaziland
Utajiri: $3.9 bilioni
8. Naguib Sawiris, Misri
Utajiri: $3.8 bilioni
9. Isabel dos Santos, Angola
Utajiri: $3.1 bilioni
10. Issad Rebrab, Algeria
Utajiri: $3 bilioni
11. Mohamed Mansour, Misri
Utajiri: $2.7 bilioni
12. Koos Bekker, Afrika Kusini
Utajiri: $2.1 bilioni
13. Allan Gray, Afrika Kusini
Utajiri: $1.99 bilioni
14. Othman Benjelloun, Morocco
Utajiri: $1.9 bilioni
15. Mohamed Al Fayed, Misri
Utajiri: $1.82 bilioni
16. Patrice Motsepe, Afrika Kusini
Utajiri: $1.81 bilioni
17. Yasseen Mansour, Misri
Utajiri: $1.76 bilioni
18. Folorunsho Alakija, Nigeria
Utajiri: $1.61 bilioni
19. Aziz Akhannouch, Morocco
Utajiri: $1.58 bilioni
20. Mohammed Dewji, Tanzania
Utajiri: $1.4 bilioni
21. Stephen Saad, Afrika Kusini
Utajiri: $1.21 bilioni
22. Youssef Mansour, Misri
Utajiri: $1.15 bilioni
23. Onsi Sawiris, Misri
Utajiri: $1.14 bilioni
24. Anas Sefrioui, Misri
Utajiri: $1.06 bilioni
25. Jannie Mouton, Afrika Kusini
Utajiri: $1 bilioni
Comments
Post a Comment