Jeshi la Polisi Zanzibar imewakamata wasambazaji 200 wa dawa za kulevya

Jeshi la Polisi Tanzania, kanda ya Zanzibar imewakamata wasambazaji 200 wa Madawa ya kulevya wakiwemo wasambaji maarufu wapatao 32 waoendelea kuhojiwa na jeshi hilo.
Akizungumza na Waandishi wa habari Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar Ramadhani Ng`anzi amesema ukatwaji huo umekuja baada ya upelelezi uliofanywa na jeshi la polisi kwa makundi matatu ya watu wakiwemo wafanyabiashara na kubahatika kuwakamata wasambazaji hao.
Hata hivyo amesema katika operesheni hiyo pia madawa ya aina mbalimbali yamekamatwa ikiwemo Heroin na Cocain Grams 3450.32,madawa mengine ni ya vidonge valium 493, Bhangi 203 na Mirungi kg46 pamoja na gari moja na pikipiki tatu ambazo zilikuwa zinatumika kusambazia biashara hiyo.
Aidha amesema  opereshen hiyo imeleta faida kubwa kwa jamii na jeshi la Polisi kutokana na kupungua kwa vigenge vya madawa ya kulevya na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Jumla ya shilingi millioni nne laki tatu na ishirini elfu zimekamatwa katika operesheni hiyo na kesi 87 zimefunguliwa tangu kuanza kwa operesheni hiyo february mwaka huu.
Na: Fat hiya Shehe Zanzibar24.

Comments

Popular posts from this blog

Tabia za Watu na Alama za Nyota

BANK LAW NOTES

ADMINISTRATIVE LAW